Kushoto ni aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini James Lembeli (Chadema) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Juma Protas wakitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo asubuhi baada ya kushinda maombi yao ya kuomba kupunguziwa gharama za kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi uliompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini,Jumanne Kishimba ambapo Lembeli alipaswa kulipa shilingi milioni 15 na badala yake Mahakama imemtaka kulipa Shilingi milioni 9 ndipo kesi ya msingi ianze kusikilizwa-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Lembeli akitoka Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga akiwa na uso wa furaha baada kuvuka kiunzi cha kwanza katika kesi namba 1 ya mwaka 2015 aliyofungua Novemba 23,mwaka huu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa CCM,Jumanne Kishimba,katika uchaguzi mkuu uliopita nchini Tanzania
Baada ya kufungua kesi hiyo James Lembeli alipaswa kulipa gharama za kesi kiasi shilingi kisichozidi milioni 15,kwa washtakiwa watatu ambao ni Jumanne Kishimba,Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Hata hivyo James Lembeli akiongozwa na Wakili Joachim Hamis kutoka Kampuni ya Mpoki and Associates Advocate aliwasilisha maombi katika Mahakama hiyo akiomba kupunguziwa gharama hiyo kwa mujibu wa sheria.
Muonekano wa jengo la Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga.
Maombi hayo yalipingwa na Mawakili watatu wa upande serikali Solomon Lwenge na Muyengi Muyengi wakiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali,Pendo Makondo,wakidai kiasi hicho Lembeli anaweza kukilipa kwa kuwa amekaa miaka 10 katika nafasi ya ubunge.
Kulia ni aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini James Lembeli (Chadema) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Juma Protas wakitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga wakitoka mahakamani.
Akisoma hukumu ya maombi hayo,Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga,Victoria Makani,amesema kuwa mbunge kwa muda wa miaka kumi hakuna mahusiano na gharama ya kesi hivyo aliridhishwa na maombi ya Lembeli ya kufikiriwa kupunguziwa gharama hiyo na kumtaka alipe shilingi milioni 9 badala ya 15 ndani ya siku 14 ndipo kesi ya msingi ipangwe kuanza kusikilizwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Juma Protas akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani
Lembeli akiwa na uso wa furaha mahakamani,ambapo tayari amelipa shilingi milioni 9 ili kesi ya msingi ianze kusikilizwa.
Mheshimiwa James Lembeli akizungumza na waandishi wa habari mahakamani ambapo ameishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki kwake katika maombi yake aliyowasilisha akidai kiwango cha awali kilikuwa kikubwa-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
BOFYA HAPA CHINI UONE VIDEO YA KIKUBWA CHUMBANI =>
TEMBELEA www.jamiiyetubongo.com KWA HABARI ZA UHAKIKA
Post a Comment