Loading...

Hii ndio sababu ya Antalyaspor kumuongezea majukumu Samuel Eto’o ya kuwa kocha mchezaji

Mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon anayekipiga katika klabu ya Antalyaspor yaUturuki Samuel Eto’o bado yupo katika kikosi hicho na anapewa nafasi kubwa. Stori zilizotoka December 15 zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Antalyaspor umempata majukumu mapya Samuel Eto’o ya kuwa kocha wa muda wa kikosi hiko.
Stori kutoka mtandao wa cameroononline.com unaeleza kuwa Eto’o atakuwa kocha mchezaji wa mpito wakati klabu yake ya Antalyaspor ikitafuta kocha mpya wa kudumu.Eto’o anatajwa kupewa nafasi hiyo huku akisaidiwa na kocha wa timu ya vijana Mehmet Ugurlu. Sababu ilyofanya uongozi ufikie maamuzi hayo ni baada ya kumfukuza kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Simsek.
samuel-etoo-antalyaspor_ggworyax55091wmgcjfr5hbrp
Eto’o ambaye amewahi kutamba kwa mafanikio katika klabu ya FC Barcelona na Inter Milan kiasi cha kutwaa taji la klabu Bingwa Ulaya akiwa na vilabu hivyo,  alijiunga na klabu ya Antalyaspor mwezi June 2015 akitokea klabu ya SampdoriaEto’o amewahi kuichezea klabu ya Chelsea ya Uingereza katika kipindi cha mwaka 2013/2014 akiwa chini ya kocha Jose Mourinho ambaye amewahi kumfundisha akiwa katika klabu ya Inter Milan.
ETOO

BREAKING NEWZZZZ!! JAMES LEMBELI AFANYA MAAJABU MAHAKAMA KUU HUKO SHINYANGA APENYA KIZINGITI CHA KWANZA



Kushoto ni aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini James Lembeli (Chadema) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Juma Protas wakitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo asubuhi baada ya kushinda maombi yao ya kuomba kupunguziwa gharama za kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi uliompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini,Jumanne Kishimba ambapo Lembeli alipaswa kulipa shilingi milioni 15 na badala yake Mahakama imemtaka kulipa Shilingi milioni 9 ndipo kesi ya msingi ianze kusikilizwa-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Lembeli akitoka Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga akiwa na uso wa furaha baada kuvuka kiunzi cha kwanza katika kesi namba 1 ya mwaka 2015 aliyofungua Novemba 23,mwaka huu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa CCM,Jumanne Kishimba,katika uchaguzi mkuu uliopita nchini Tanzania
Baada ya kufungua kesi hiyo James Lembeli alipaswa kulipa gharama za kesi kiasi shilingi kisichozidi milioni 15,kwa washtakiwa watatu ambao ni Jumanne Kishimba,Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Hata hivyo James Lembeli akiongozwa na Wakili Joachim Hamis kutoka Kampuni ya Mpoki and Associates Advocate aliwasilisha maombi katika Mahakama hiyo akiomba kupunguziwa gharama hiyo kwa mujibu wa sheria.
Muonekano wa jengo la Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga.
Maombi hayo yalipingwa na Mawakili watatu wa upande serikali Solomon Lwenge na Muyengi Muyengi wakiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali,Pendo Makondo,wakidai kiasi hicho Lembeli anaweza kukilipa kwa kuwa amekaa miaka 10 katika nafasi ya ubunge. 
Kulia ni aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini James Lembeli (Chadema) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Juma Protas wakitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga wakitoka mahakamani.
Akisoma hukumu ya maombi hayo,Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga,Victoria Makani,amesema kuwa mbunge kwa muda wa miaka kumi hakuna mahusiano na gharama ya kesi hivyo aliridhishwa na maombi ya Lembeli ya kufikiriwa kupunguziwa gharama hiyo na kumtaka alipe shilingi milioni 9 badala ya 15 ndani ya siku 14 ndipo kesi ya msingi ipangwe kuanza kusikilizwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Juma Protas akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani
Lembeli akiwa na uso wa furaha mahakamani,ambapo tayari amelipa shilingi milioni 9 ili kesi ya msingi ianze kusikilizwa.
Mheshimiwa James Lembeli akizungumza na waandishi wa habari mahakamani ambapo ameishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki kwake katika maombi yake aliyowasilisha akidai kiwango cha awali kilikuwa kikubwa-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

BREAKING NEWS:.MAJINA YA MAWAZIRI WAPYA,.RAIS MAGUFULI ATANGAZA RASMI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI..HILI BARAZA KWELI KIBOKO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

Wizara 18, mawaziri 19. Wizara nyingine hazitakua na manaibu waziri. Hakuna siku za retreat/semina elekezi (saving 2billion)

1wizara ya ofisi ya raisi tamisemi utumishi na utawalabora (Simbachawene, Angela Kairuki Naibu, Japho selemani

Muungano na mazingira ( Makamba, Naibu Mpina)

Waziri mkuu withvijana na ajira na walemavu  (Jenista Mhagama, Naibu Dr Abdalla Possi, Mavunde)

Kilimo, mifugo na uvuvi (Mwigulu Nchemba Naibu williumNasha

Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano (............., Naibu Edwin Ngonyani)

Fedha na Mipango (............, Ashanti Kijaji)

Nishati na madini ( Muhongo, Naibu Medadi)

Katiba na Sheria (Mwakyembe)

Mambo ya nje, Afrika Mashariki (Mahiga, Naibu Kolimba

Ulinzi (Hussein Mwinyi)

Mambo ya ndani (Charles Kitwangwa)

Ardhi nyumba na makazi (Lukuvi, Naibu Angelina Mabula)

Maliasili na Utalii ( ............., Naibu Makanye)

Viwanda na uwekezaji ( Majage)

Elimu, sayansi na ufundi ( ............., Naibu Manyanya)

Maendleeo ya jamii (Ummy Mwalimu, Kigwangala)

Habari, utamaduni, wasanii na michezo ( nnauye, Naibu Wambura)

Maji (Prof Makame, Naibu Kamwele)

BREAKING NWZZ: ZITTO KABWE ATOA KAULI KUHUSU WANAHOJI KWANINI HAKUTUMBUA MAJIPU YA BANDARI WAKATI AKIWA MWENYEKIT WA PAC

LOWASSA: MAGUFULI ANATEKELEZA HOJA ZANGU NA CHADEMA


Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Magufuli imeanza kuzifanyia kazi hoja zake alizozieleza wakati wa uchaguzi.
Lowassa aliyasema hayo jana jijini Arusha alipokuwa akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni.
Lowassa aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kumuachia huru Sheikh Issa Ponda na kuiomba kuliangalia pia suala la mwanamuziki, Nguza Vicky (Babu Saye) na mwanae.
“Haya mambo ndiyo tuliyoyaema wakati wa kampeni, sasa namuona Magufuli ameanza kuyatekeleza. Sasa nawaomba angalau wawe wanasema hizo ni sera za Lowassa na Chadema na wanapozitumia basi wawe wanatushukuru,” alisema Lowassa.
Kauli hiyo ya Lowassa iliungwa mkono na waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye aliwataka pia wananchi wa jimbo hilo kumchagua Lema ili aende bungeni akatumbue majipu ambayo yanapeleka damu kwenye mishipa ya moyo, majipu ambayo alidai CCM haiwezi kuyatumbua.

TRA YAGOMEA WAMILIKI WA MAKONTENA YALIYOTOROSHWA BANDARINI BILA KULIPIWA USHURU.


Mmamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewagomea kulipa kodi bila adhabu baadhi ya wamiliki wa makontena, ambayo yalitoroshwa kwenye bandari kavu bila kulipiwa kodi.
Badala yake, TRA imewapelekea hati ya malipo inayowataka wafanyabiashara hao, kuhakikisha wanalipa kodi hiyo na adhabu ndani ya siku saba, la sivyo watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wamiliki wa makontena hayo, kuiomba TRA kuwasamehe kulipa adhabu waliyopewa badala yake waruhusiwe tu kulipa kodi stahiki ya Serikali.
Jumla ya makontena 349 yalitoroshwa katika bandari kavu bila kulipa kodi na kuikosesha Seri kali mapato ya Sh bilioni 80.
Wafanyabiashara hao, pia wameomba waruhusiwe kulipa kodi wanayotakiwa kulipa kidogo kidogo kwa madai kuwa wengine hawana uwezo wa kulipa kiasi hicho cha fedha kutokana na kutapeliwa na mawakala wao waliowatumia kwenda kulipa kodi hiyo.
Wakizungumza na mwandishi, baadhi ya wafanyabiashara hao walisema agizo la Dk Magufuli alilotoa Desemba 3, mwaka huu kuwa linawataka walipe kodi hiyo ndani ya siku saba.
Lakini wafanyabiashara walisema nyaraka za malipo walizopelekewa na TRA, zimewataka kulipa kodi na faini kwa pamoja wakati hizo siku saba alizotoa Dk Magufuli hazijamalizika.
Wafanyabiashara hao wanadai kuwa walishalipa kodi hiyo kupitia kwa wakala wao, kama taratibu za TRA zinavyowataka kuwatumia mawakala wa bandarini kulipa kodi, lakini kwa bahati mbaya wakala huyo hakufikisha kodi hiyo serikalini.
Walidai kuwa walifuatilia nyaraka za kodi kwa wakala wetu, lakini akawa anawaambia wasubiri.
“Tunaomba hii adhabu tusamehewe, kwani sio kosa letu ila tuko tayari kulipa kodi halali ya Serikali, lakini wakala wetu ndiye katuingiza kwenye matatizo haya na yeye tayari ameshatoroka,” aliongeza mfanyabiashara huyo.
Katika nyaraka za kodi ambazo TRA imewapelekea, kontena moja linatakiwa kulipiwa ushuru wa Sh milioni 40.5 ndani ya siku saba na adhabu ya Sh milioni 28.3. Hivyo jumla wanatakiwa kulipa Sh milioni 68.8 kama ushuru na adhabu.
Akizungumza na mwandishi kuhusu madai hayo ya wafanyabiashara, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema adhabu walizoandikiwa wafanyabiashara hizo, wanatakiwa kuzilipa pamoja na kodi stahiki ndani ya siku saba.
Alisema wamewawekea adhabu hiyo kutokana na kitendo chao cha kuiibia Serikali na kwa taratibu za nchi, walitakiwa wawe mahabusu sasa hivi, lakini wametakiwa kulipa ushuru wa Serikali wakati wakiwa nje; hivyo wanastahili kulipa kiasi hicho cha fedha kama adhabu ya kukwepa kodi.
“Hawa walitakiwa kukamatwa na kuwekwa ndani, walitoa kontena nje ya utaratibu, adhabu hiyo ni ya kutoa makontena bila kulipa kodi,” alisema Kayombo. “Wakishindwa kulipa ndani ya muda huo tutawakamata tena na kuwafikisha mahakamani,” alieleza.
Kayombo alifafanua kuwa siku saba hizo walizopewa wafanyabiashara hao ni kusamehewa kutoshitakiwa mahakamani na sio kusamehewa kulipa adhabu wakati tayari walishakiuka taratibu.
Alisema wafanyabiashara hao, wachague kulipa ndani ya siku saba wasishitakiwe au waache ili wakutane na rungu la dola la kufikishwa mahakamani.
Alisema hadi sasa TRA imeshakusanya Sh bilioni 9.4 kati ya Sh bilioni 80 zinazotakiwa kulipwa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara hao waliokwepa kodi.
Newer Posts
© Copyright JAMII YETU | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top