Mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon anayekipiga katika klabu ya Antalyaspor yaUturuki Samuel Eto’o bado yupo katika kikosi hicho na anapewa nafasi kubwa. Stori zilizotoka December 15 zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Antalyaspor umempata majukumu mapya Samuel Eto’o ya kuwa kocha wa muda wa kikosi hiko.
Stori kutoka mtandao wa cameroononline.com unaeleza kuwa Eto’o atakuwa kocha mchezaji wa mpito wakati klabu yake ya Antalyaspor ikitafuta kocha mpya wa kudumu.Eto’o anatajwa kupewa nafasi hiyo huku akisaidiwa na kocha wa timu ya vijana Mehmet Ugurlu. Sababu ilyofanya uongozi ufikie maamuzi hayo ni baada ya kumfukuza kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Simsek.
Eto’o ambaye amewahi kutamba kwa mafanikio katika klabu ya FC Barcelona na Inter Milan kiasi cha kutwaa taji la klabu Bingwa Ulaya akiwa na vilabu hivyo, alijiunga na klabu ya Antalyaspor mwezi June 2015 akitokea klabu ya Sampdoria. Eto’o amewahi kuichezea klabu ya Chelsea ya Uingereza katika kipindi cha mwaka 2013/2014 akiwa chini ya kocha Jose Mourinho ambaye amewahi kumfundisha akiwa katika klabu ya Inter Milan.